Habari za Mastaa

Video fupi ikimuonyesha Rais Obama akicheza wimbo wa Sauti Sol Kenya.

on

Sauti Sol ObamaSauti Sol ni kundi maarufu la muziki kutokea nchini Kenya ambalo limefanikiwa kuvuka hata mipaka na kuteka kwenye nchi jirani kama Tanzania, Rwanda, Burundi na nchi nyingine za Afrika mpaka kupelekea kuwa nominated kwenye tuzo kubwa kama za MTV na BET 2015.

Kundi hili lilipata mwaliko maalum wa kwenda kuimba Ikulu ya Kenya kwenye party ya kumkaribisha Rais Barack Obama wa Marekani ambaye baba yake mzazi ni mzaliwa wa Kenya.

Tazama kwenye hii video fupi hapa chini jinsi Sauti Sol walivyokuwa wakiperfom na baadae Rais Obama na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuungana nao kucheza.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments