Muigizaji na staa Irene Uwoya amekwazika na maneno ya baadhi ya mashabiki kumsema kuwa ana tabia ya kuringa huku wengine wakidai kuwa anavalishwa nguo bure ili kupromote biashara za watu.
Staa huyo ameutumia ukurasa wake wa instagram kuwajibu wale wote wanaodhani kuwa anafanya hivyo kwa ajili ya kupromote kazi za baadhi za wafanyabiashara na kusisitiza kuwa kama kila mtu angekuwa anafanya hivyo basi ingekuwa ngumu mtu kupata faida.
“Jaman kwanza za asubuh!!!naomba tuelewane hapa kitu naona dm watu wananambia navalishwa bure najishauwa sijui nin…hiv kwanin mnapenda kunifanya niongeee jamani hii naongea ya mwanzo na mwisho siongei tenaaa!!!?
“Hivi ata siku moja sijawah kupewa kitu bure ili ni mtag mtu…mim naamini ukitaka kumuungisha mtu au ku-support biashara ya mtu nunua afu tag na sio bure jamani na yeye anatumia pesa kufanya biashara,”
“Sasa wote tukipewa bure faida atapata wap? sikatai kama wasanii tumetumia nguvu na mda mwingi kutengeneza jina lakin kuna vitu too much jamaniii kama mtu anataka mtangazie biashara apo sawa mtaelewana”
“Lakin kuna wasanii wanapenda kitonga hatari…yani mtu anaenda kabisa dukani ananunua Nguo anagoma ku-tag kisa kanunua na ukitaka tag basi apewe bure jamani tuwe na huruma sometimes basi ata upunguziwe kidogo lakin sio bure kabisa kiukweli inauma ni basi tu hamna namna basi hata upewe mara moja kama star lakin mtu kila ukiombwa upewe bure ndo una tag jaman mimi na nunua sababu nafanya biashara naelewa awez kuja mtu Bar kwangu achukue pombe bure kisa ata ni tag no hiyo sio support nikurudishana nyuma yani mtu kabisa ni star lakin atakitu cha 50,000 unataka bure ili utag”
“Jamani waoneeni huruma hawa wafanya biashara wadogo jamaniii sio powa naamini ata ungekuwa wewe usingependa kutowa bure mtu akitaka utangaze biashara yake kwakipindi flani hiyo ni ishu nyingine lakin eti ukinunua u tag mtu mpaka akupe bure ni tabia mbaya kama kweli wewe star nunua na tag hiyo ndio maana halisi ya support na sio bure!!! Kama nimewakosea jamaniii samahanini soreniiii🙏”
“SIWEZI KUAMBATANA NA DOGO JANJA / SITAKI VYA BURE ” – UWOYA