Staa wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown anashikilia headlines za burudani na album yake mpya, ROYALTY.
Nimekutana na interview aliyofanya Chris siku chache zilizopita na humo ndani amegusia vitu vingi ikiwemo mchango wa station za radio kwenye muziki wake, mtazamo wake wa kuwa na kuitwa superstaa na maisha aliyoishi akiwa jela.
Haya ndio aliyoyasema Chris Brown kupitia interview yake na Power 106.5 Radio ya Los Angeles, Marekani…
Mchango wa station za radio kwenye muziki wake: “Radio ndio sababu pekee inayoniwezesha mimi kuweka headlines, sababu pekee inayonifanya mimi niendelee kufanya muziki… Naiheshimu sana radio kwa sababu wamekuwa supporters wangu wakubwa sana pia radio imesaidia kusukuma muziki wangu kwa asilimia kubwa sana, ni kwa sababu yao naendelea kusikika kwenye nyumba na sebule za watu, ni kwa sababu yao pia bado napata na kufanya interviews…“
Mtazamo wake kuhusu kuitwa superstaa: “Kwa muda mrefu sana watu tofauti duniani wamejiwekea picha kichwani ya jinsi gani ambavyo staa anatakiwa kuwa, kuonekana, kuongea au hata kuvaa na kwa bahati mbaya sana sisi tunaoitwa ‘superstars’ tumejifunga kwenye hii mitazamo na kuiacha itutafsiri… hii sio sawa kwani mimi nipo kama wengine wote hivyo nina haki ya kuwa mtu wa kawaida, kufanya vitu bila kuwekewa lebo zozote mgongoni kwa sababu mimi ni binadamu pia“.
Kuhusu maisha aliyoishi akiwa jela: “Jela maisha sio mazuri kabisa… haswa chakula! Chakula cha jela ni kibaya mno lakini uzuri ni kwamba kila jumapili mtu alikuwa anaweza kuagiza chochote akitakacho kutoka nje ili mradi tuu vitu hivyo visizidi dola 200 (kama Tsh 400,000 za Tanzania) unayopewa na Bodi ya Gereza husika… sasa mimi nilikuwa nasubiria kweli ifike jumapili niagize vyakula vyangu na ndio maana nilivyotoka jela nilikuwa nimenenepa sana…“
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.