Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Kwenye Muziki kuna njia nyingi sana za kukuingizia mkwanja. SANAA PANA MSIBANANE.
— Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Unaweza ukasimama kama Songwriter/Composer/Producer/Engineer na bado ukajiingizia pesa ya kujikimu na maisha yakaendelea. — Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Muandishi wa nyimbo ukijiwekea utaratibu mzuri wa mgawanyo wa mapato kati yako na unaowaandikia itakunufaisha hata isipokuwa sasa baadae.
— Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Lakini hakikisha kuna makubaliano ya kimaandishi kati yako na unaemuandikia wimbo. La sivyo imekula kwako. — Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Pamoja na Changamoto za kimfumo katika kuisimamia Biashara ya Sanaa, nisikudanganye ukijipanga hela ya kuyasogeza mambo mengine yaende ipo.
— Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Na ili mambo yawe vizuri zaidi ni lazima wafanya biashara ya sanaa tuwe katika mifumo rasmi ya mamlaka zinazosimamia kazi zetu. — Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Japokuwa kwenye mamlaka husika wamelala usingizi wa pono, kelele zetu tusizipigie nje. Kelele za ndani zitawaamsha kama si kuwakimbiza.
— Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Katika zama hizi huwezi kusimamia Biashara ya Sanaa kwa mtindo uliokuwa unautumia enzi zile unasimamia Kikundi cha ngoma au maigizo. — Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Ndani ya Baraza, Vyama, Mashirikisho tuwe na watu wenye kutambua vyema hilo. Wenye kwenda na wakati na mbinu mpya kulingana na muda.
— Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Pamoja na yoteee, tambua nafasi yako katika sanaa. Sanaa siyo uimbaji tu SANAA PANA. — Lameck Ditto (@Lameckditto) January 2, 2015
Mwaka 2015 ni mwaka wa #Mabadiliko. Watanzania wanataka #Mabadiliko. WanaCCM tutafanya #Mabadiliko makubwa kuanzia sera, fikra na viongozi!
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 2, 2015
2015 haitokuwa mara ya kwanza kwa CCM kuengua watoa rushwa wasifikie kupigiwa kura na wajumbe. Kanuni za uchaguzi za CCM ziko wazi. — Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 2, 2015
Kaka Mourinho,ujumbe wa kufungulia mwaka,kiburi si maungwana..Twende tukaswali..Ijumaa Kareem..
— Hamis Mwinjuma (@MwanaFA) January 2, 2015
Ukitaka usiende jela bongo iba pesa za umma sio kuku mtaani. — Izzo_bizness (@Izzo_bizness) January 2, 2015
Uendapo kufanya ibada, zingatia ni amrisho la Muumba wako. Usifikirie adhabu wala thawabu za ibada hiyo. Juma’a Qarym.
— Noorah (@BabaStylz) January 2, 2015
Kusema gesi itafikisha Tanzania nchi ya PATO LA KATI mwaka 2025 ni UONGO. Acheni kuchezea matarajio (expectations) ya WaTz. Ombeni radhi — Reginald Mengi (@regmengi) January 2, 2015
Simba 6 wauliwa nje ya hifadhi ya Tarangire na wamaasai wapatao kama 100 baada ya simba hao kuvamia mifugo yao. Ni kinyume cha sheria.
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 1, 2015
Elimu ya uhifadhi inapaswa kuwa sehemu ya mitaala ya elimu yetu na kwa pamoja tutunze na kuhifadhi rasilimali tulizobarikiwa kama nchi. — Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 1, 2015
Hatua kali zinachukuliwa kwa yoyote anayekwenda kinyume na sheria za uhifadhi
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 1, 2015
Elimu ya uhifadhi inapaswa kuwa sehemu ya mitaala ya elimu yetu na kwa pamoja tutunze na kuhifadhi rasilimali tulizobarikiwa kama nchi. — Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 1, 2015
Hatua kali zinachukuliwa kwa yoyote anayekwenda kinyume na sheria za uhifadhi
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 1, 2015
Kila mtu atapata kile alichoandikiwa na Mungu, Hata ufanye kazi kiasi gani kilichopangwa kwako hakitabadilika,Ridhika na ushukuru kwa moyo 1 — Batuli_Actress (@Batuli223) January 2, 2015
I’m glad to say I’ve officially decided to quit music….Wishing all the best to the slaves and victims of Music industry. #2015
— I’mNotStupid (@NikkiZohan) January 2, 2015
Nitaziachia tracks zangu zote ambazo hazijatoka for free then SITOINGIA TENA STUDIO kufanya wimbo(MUZIKI BASI) #My_decision_2015 — I’mNotStupid (@NikkiZohan) January 2, 2015
The Industry is designed to frustrate the cats with high degrees of talents and intelligence. Ngwea,Langa,Geez mlale pema wanangu.
— I’mNotStupid (@NikkiZohan) January 2, 2015
I will remain as a music fan…and u guys need to find me some hip hop heads to listen to…asanteni. — I’mNotStupid (@NikkiZohan) January 2, 2015
Tusije kushikiana bunduki bure maana milango ya kutoka kimaisha ni mingi na muziki ni burudani na biashara sio vita.
— I’mNotStupid (@NikkiZohan) January 2, 2015
Kama Mzee kashindwa na Escrow itakuwa Muziki? — I’mNotStupid (@NikkiZohan) January 2, 2015
Mpaka lini tutauza UNGA kwa kivuli cha kuwa WASANII?
— I’mNotStupid (@NikkiZohan) January 2, 2015
CloudsFM
1.CLOUDS TV INTERNATIONAL YAZINDULIWA RASMI DUBAI Hongera kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bw Joseph Kusaga ndoto yake imekuwa kweli sasa Clouds TV International kuwa kituo cha kwanza cha Television cha Kiafrika kuonekana nchi zote za Falme za Kiarabu. #TunakufunguliaDuniaKuwaUnachotaka
- JK:MAJANGILI WAKAE MBALI RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali itapambana kufa na kupona kuhakikisha ujangili na biashara haramu za wanyamapori zinakomeshwa. Ameonya kuwa huu mwaka utakuwa wa mapambano makali zaidi ya miaka iliyopita katika kukabiliana na majangili kwenye hifadhi za taifa na mbuga za wanyama nchini. Kwa mujibu wa Rais Kikwete mwaka jana , ndovu 114 waliuwawa, ikilinganishwa na ndovu 219 waliouwawa mwaka 2013 na ndovu 473 mwaka 2012, huku majangili 1,354 wamekamatwa na pembe za ndovu 542 na silaha mbalimbali 184 nazo zilikamatwa.
Chid Benz:Nakanusha habari za Nikki mbishi kuacha mziki,nimeongea nae kama kaka na kumgusia mengi,najua amenielewa na nimemwambia asikubali wale wanaomkubali waanze kukubali wengine.mimi nimekumbana na vingi na watu weengi waliaminishwa kama nimeshushwa kimziki,jimefanyiwa mengi ambayo kwa muda ule nsingeweza kuelezea kila mtu nini kinaendelea,so if kikitokea kibaya kinatangazwa mpk kwenye taarifa za habari mbona mziki hauchezwi?ningekua sina nguvu hio nisingesumbua watu kuniweka front page..but bado nipo na nimekomaa.na naishi na naona wanaopewa kipaumbele na najua bado mimi ni mimi.Iron
HATIMAE KAKA DUDUBAYA NA KAKA MR.NICE WAMALIZA BEEF!! A photo posted by dully sykes (@princedullysykes) on
Thanks bro Chuma @chidbeenzchuma A photo posted by Baba Malcolm (@nikkimbishi) on
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook