Habari za Mastaa

Baada ya Future kumshambulia Ciara kwenye Twitter… kambi ya Ciara haijamuacha bure!

on

Mvutano kati ya Future na Ciara juu ya malezi ya mwanao, ‘Baby Future’ umezidi kuwa mkubwa, baada ya Future kumshambulia vikali Ciara, kambi ya Ciara haijakaa kimya wao pia wameongea na kueleza upande wao wa stori.

LOS ANGELES, CA - FEBRUARY 09: Recording artists Future (L) and Ciara arrive at the 55th Annual GRAMMY Awards Pre-GRAMMY Gala and Salute to Industry Icons honoring L.A. Reid held at The Beverly Hilton on February 9, 2013 in Los Angeles, California. (Photo by Larry Busacca/Getty Images for NARAS)

Kwa mujibu wa mtandao wa E!News wa Marekani, kambi ya Ciara imepinga tuhuma za Future kupitia page yake ya Twitter siku ya Jumatatu January 4 2016, kuwa Future inabidi apitie mlolongo wa Wanasheria ili tu kupewa ruhusa ya kumuona mwanae…

>>> “ Future ameshawahi kumwambia Ciara kuwa anamuombea mabaya kwenye kila kitu atakachokifanya, na hiyo ni roho mbaya… amejaa na wivu na anashindwa kuendelea na maisha yake na kushirikiana vizuri na mwenzake kwenye kumtunza mtoto wao vizuri…“<<< Chanzo cha karibu na Ciara kiliwaambia E!News.

cx3

Chanzo cha karibu na Ciara pia kimesisitiza kuwa Ciara hajawahi kumzuia rapper huyo kumuona mtoto wao na wala hajawahi kutoa kiasi cha pesa alichodai anatoa kwa ajili ya malezi ya mtoto wao.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE


Soma na hizi

Tupia Comments