Msanii wa filamu, Faiza Ally ambae time hii amefunguka kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram aliweka video yenye dakika 3 ikiashiria akisikika akisema anahitaji mwanaume wa kuishi nae kwani mahusiano ya mbali yamemshinda.
Kupitia Video hiyo alisikika mrembo huyo na kusema ‘Kwanza mara Leo nimetamani ningekuwa na Boyfriend ama Mume kwasababu kuna mtu ninasababu nae za kibiashara amekuwa ananipa wakati mgumu sana ananisumbua’– Faiza Ally
‘Siko single Ila Baba Lily yuko mbali na hii Corona, mahusiano ya mbali ni magumu sana, nimetamani kuwa na Mwanaume ndio maana nafikiria ni wakati wangu kwa sasa wa kutafuta mtu sahihi sasa nimechoka’– Faiza Ally