Habari za Mastaa

Mume wa Ciara atajwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi, afanya hiki siku ya Mama Duniani (+video)

on

Mchezaji wa timu ya Seahawks Ligi ya National Football League (NFL)  Russell Wilson amechukua headlines siku ya jana May 12,2019 baada ya kumzawadia mama yake nyumba ikiwa ni siku ya maadhimisho mama duniani na alipost video kupitia ukurasa wake wa instagram.

Inaripotiwa kuwa mchezaji huyo ambaye ni mume wa Ciara, alisaini mkataba wa miaka minne dola za Kimarekani Milioni 140 sawa na zaidi ya shilingi  Bilioni 322 za Kitanzania na timu yake ya Seahawks ya Ligi ya National Football League  (NFL) siku kadhaa zilizopita kutokana na mkataba huo unamfanya Russell kutajwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye ligi hiyo kwa sasa.

“Kwa miaka yote hii haujawahi kuniomba kitu, kitu ambacho ulikua ukihitaji ni mimi kukupenda, asante kwa kutupenda hii ni kwaajili yako, Nakupenda mama” >>>aliandika Russell

VIDEO: ULIPITWA NA MAJIBU YA LINAH BAADA YA KUULIZWA ANAMZUNGUMZIAJE AMINI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.

Soma na hizi

Tupia Comments