Habari za Mastaa

VIDEO: Stonebwoy amchomolea bastola Shatta Wale stejini

on

Fahamu kuwa usiku wa Jumamosi May 18,2019 zilifanyika tuzo za 20 za VGMA (Vodafone Ghana Music Awards) nchini Ghana na baadae kuliibuka mzozo kutokana na ugwaji wa tuzo kushindwa kumtanganza mshindi wa kipengele cha Msanii bora wa mwaka.

Baada ya Mwimbaji Stonebwoy kutangazwa kwa mara ya 5 mfululizo sasa kama mshindi wa kipengele cha msanii bora wa muziki wa Reggae/Dancehall inaonekana mwimbaji mwenzake Shatta Wale hakuridhishwa na matokeo hayo na kuamua kuvamia stage na kuanza kufanya vurugu, kitendo hicho kilimpelekea Stonebwoy kuchomoa bastola jukwaani.

Inaelezwa kuwa sababu ya vurugu hiyo ni kuwa wawili hao wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu sasa huku chanzo cha bifu lao kikiwa hakijatajwa lakini imearipotiwa kuwa polisi wanamshikilia Stonebwoy kwa kitendo hicho na hakuna mtu aliyejeruhiwa.

VIDEO: CHEKI STYLE MPYA BALAAH ZA CHALII ‘R’ CHUGGA, “MBELE MBELE YAO, KUSOMA NI USIKU”

Soma na hizi

Tupia Comments