Ad

Habari za Mastaa

Billinas kuhusu kuzifanyia remix nyimbo za Godzilla (255)

on

Staa wa Bongofleva Billnas leo July 14, 2017 amefunguka na kuzitaja baadhi ya nyimbo za Godzilla ambaye amekana kuwa mrithi wake akisema hawezi kurithi pengo la mtu aliye hai na kukiri kuwa anatamani kuzifanyia Remix baadhi ya ngoma za Godzilla.

Akizungumza kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM Billnas amesema nyimbo za Godzilla anazoweza kuzifanyia remix ni ‘Nataka’ na ‘King Zilla’ kutokana na ilivyopangwa mistari yake na namna Godzilla alivyojinadi vizuri kitu kilichomvutia.

>>>“Ngoma za Godzilla ninazoweza kuzifanyia remix labda mbili; Nataka na King Zilla, huu ni wimbo ambao una mistari inayoweza kunigusa. Ni wimbo ambao alijinadi vizuri mfano, ‘Kila baada ya dakika tatu na change dress code’ ‘Nacheka kwa dharau Life is Simple’. Kwa hiyo ni wimbo ambao ni rahisi kwangu kuufanyia remix kwa kuwa naujua mstari baada ya mstari halafu beat yake Makochali aliumiza zaidi.” – Billnass.

EXCLUSIVE: Babu Tale kaeleza kuhusu collabo ya Tekno na Madee 

Soma na hizi

Tupia Comments