Habari za Mastaa

Kifo cha mrembo mchekeshaji kilichoshutua mastaa mtandaoni

on

Kifo cha mrembo Martha aliyekuwa akijishughulisha na shuguli za Uchekeshaji, MC na hata kuigiza kimeshutua baadhi ya watu wakiwemo mastaa mtandaoni waliokuwa wakimfahamu kutokana na kuwa kifo chake kuwa cha gafla baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Inaelezwa Martha alikuwa akiugua uti wa mgongo kwa muda mrefu na ndipo kisha kuugua maleria kali na awali alilazwa katika hospitali iliyopo Sinza Palestina na kisha kuhamishwa kupelekwa katika hospital nyingine ambapo ndipo umauti ukamkuta.

Enzi za uhai wa Martha alishawahi kufanya kazi nyingi ikiwemo kuwa moja ya wachekeshaji waliokuwa wakifanya Standup comedy ya ‘Cheka tu’ inayofanyikaga kila ijumaa ya mwisho wa mwezi, pia alishawahi kushiriki kwenye baadhi ya kazi za wasanii wa bongofleva kama kwenye video ya Whozu ya ‘Roboti’

Baadhi ya watu maarufu wameonesha kuguswa na kifo hicho na kupost haya kupitia kurasa zao za Instagram..

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments