Habari za Mastaa

Hii ndio headline mpya ya Jay Z na Beyonce.

on

jayMoja kati ya familia maarufu hivi sasa kwenye kiwanda cha burudani ni ya Mr and Mrs Carter ambao wote wawili wana-status kubwa kwenye muziki.

Mwaka jana wote wawili walitoka na vitu vipya kwenye soko la muziki kwa kuanza kuuza album zao kwa njia tofauti kabisa.

Jay Z alitoa album yake ya Magna carta holy grail kupitia app ya Samsung na Beyonce alitoa ghafla bila hata promotion album yake kupitia iTunes.

Mambo haya na mengine mengi kama kushinda tuzo,tours, kukusanya mashabiki wengi,ushawishi kwenye game ya muziki,mikataba na makampuni mbalimbali imeshawishi Billboard Magazine kuwataja kama most powerful couples kwenye muziki.

Unadhani kwa Tanzania most powerful couple kwenye kiwanda chote cha burudani(muziki.michezo,movie na vingine) watakuwa nani na nani?…Comment.

 

Tupia Comments