Habari za Mastaa

Pichaz & Video: Staa wa tenis duniani kwenye headlines

on

harusi2Ukiachilia mbali Staa wa mchezo wa tenis duniani Serena Williams kuna huyu mwingine Andy Murray ambaye naye ni miongoni mwa mastaa wanaofanya vizuri katika mchezo huo duniani.

Andy Murray sasa ameingia kwenye ukurasa mpya wa maisha baada ya kufanya uamuzi wa kufunga ndoa  na mpenzi wake wa siku nyingi Kim Sears.

Katika harusi hiyo ya kifahari iliyofanyika nyumbani kwao Uingereza, ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wachezaji wenzake sambamba na vyombo vya habari ambavyo vilifanikiwa kuchukua tukio zima.

Moja ya vitu ambavyo vilivutia harusi hiyo ni pamoja na jinsi bwana harusi Murray alivyokuwa amevaa jambo ambalo si rahisi kukutana nalo kwenye harusi nyingi.

harusi

harusi2

harusi3

harusi4

harusi5

https://www.youtube.com/watch?v=qcPdepUUVp8

 

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments