Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Aika na Nahreel mbioni kumleta mtoto wao wa pili

on

Mwimbaji Aika kutokea kwenye kundi la Navy Kenzo anatarajia kupata mtoto wake wa pili siku chache zijazo, Aika pamoja na Nahreel wameanika good news hizi kupitia kurasa zao za instagram huku mastaa tofautofauti wameonekana kwapongeza kwa kitu hicho.

Tayari jinsia pamoja na jina la mtoto wao wa pili limeshaachiwa hadharani, fahamu kuwa mtoto huyo wa kiume ataitwa Jamaika ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Gold ambaye alizaliwa Jumamosi ya December 9 2017.

“Zimebaki siku chache JAMAIKA aungane na sisi Inshallah 🙏🙏🙏 #BabyBoy #9months” >>> aliandika Aika

Nikukumbushe tu kuwa Aika na Nahreel ambao ni wasanii wanaounda Kundi la Navy Kenzo wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka kumi hadi sasa na hatimae mwaka huu 2019 wanamkaribisha mtoto wao mwingine wa pili.

FULL VIDEO: NANDY ALIVYOIMBA WIMBO KWAAJILI YA RUGE MUTAHABA SUMBAWANGA

Soma na hizi

Tupia Comments