Habari za Mastaa

Nollywood kuibeba Nigeria kiuchumi? Ripoti ya Umoja wa Mataifa Tume ya Kimataifa ya Biashara imeeleza haya!

on

niijaa

Nimekutana na makala inayozungumzia ukuwaji wa tasnia ya filamu nchini Nigeria, je unajua ya kuwa Nigeria inatengeneza zaidi ya movie 50 kwa wiki moja tu? Na ina toa ajira kwa watu zaidi ya millioni moja ikiwa ni Sekta ya pili inayo ongoza kwa kutoa ajira huku Sekta ya kilimo ikiongoza?!

12 Kate Henshaw, Rita Dominic, Stephanie Linus & Omotola Jalade-Ekeinde

Inawezekana hujui mengi sana kuhusu Nollywood ya Nigeria, nimefanya jitihada ya kukusogezea kile nilichokipata kuhusu Industry hiyo, yafuatayo yatakuacha hoi mtu wangu!

zzzzz

Movie zinazotengenezwa Nollywood sasa hivi zimefika levo za kuuzwa kimataifa, wakiwa wanatengeneza zaidi ya movie 500 kwa mwezi za stori zinazohusu mapenzi, visa na visasi, comedy na uchawi, Nigeria pia ni nchi ambayo kwa wiki tu ina uwezo wa kutengeneza movie 50 na 30 zenye vigezo vya kimataifa.

Nollywood-cnn

Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa Tume ya Kimataifa ya Biashara inasema kwamba tasnia ya filamu Nigeria inachangia karibia dola Millioni 600 kwenye pato la taifa kwa mwaka ikiwa ni tasnia inayotengeneza zaidi ya movie 1,200 kwa mwaka na pia ni tasnia ya pili kwa ukubwa wakiongozwa na India.

Ripoti hio imeweka wazi kuwa Nollywood ni sekta kubwa ya pili inayoongoza kwa kutoa ajira Nigeria ikiongozwa na sekta ya kilimo.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments