Rapper Meek Mill ameiomba Mahakama kumtoa kwenye shitaka la mauaji ambalo familia moja ya Graves ilimuingiza baada ya vijana wao Jaquan Graves na Travis Ward kupoteza maisha kwenye tamasha lake mjini Connecticut mwaka 2016.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Blast’ umeripoti kuwa nyaraka kutokea Mahakama zimeorodhesha kuwa Meek Mill amedai hana hatia na shambulio lililofanyika na kusababisha vifo vya vijana hao huku upelelezi uliofanywa na Polisi ulidai kuwa vijana hao walihusika kwenye shambulio hilo kama washambuliaji.
Meek Mill amezidi kuiomba Mahakama kutoa jina lake kwenye shitaka hilo haraka iwezekanavyo huku akidai kuwa sio sahihi kumtuhumu yeye peke yake kati ya watu watatu akijumuisha kampuni ya Oakdale Musical Theatre pamoja na Live Nation citing ambao walitakiwa kuhusika kwenye suala zima la ulinzi na usalama.
VIDEO: MREMBO POSHY AMEJIBU KUDAIWA KUTOKA NA MWANAUME ANAYEDAIWA NI WA ZARI THE BOSS LADY