Leo September 21, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ‘DPP’ kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi yake ya kula njama ili kutenda kosa iliyodumu kwa miaka minne na nusu.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa wanaomba kesi hiyo iondolewe chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kilichofanyiwa marekebisho 2002.
Kishenyi ameeleza kuwa sababu ya kuomba shauri hilo liondolewe ni kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi hiyo ambapo baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amesema ameifuta kesi hiyo na mshtakiwa (Lwakatare) yupo huru.
Awali, DPP aliondoa maombi yake dhidi ya Lwakatare, kuhusiana na shtaka la ugaidi dhidi yake katika Mahakama ya Rufaa ambayo aliyafungua akiomba kibali cha kufungua maombi ya mapitio kuhusiana na uamuzi wa Mahakama Kuu kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi.
Katika kesi hiyo, Lwakatare na mwenzake Ludovick Rwezaura, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi kwa lengo la kumdhuru kwa sumu aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.
Mashtaka mengine yalikuwa ni ya ugaidi, wakidaiwa kuandaa mikutano ya kupanga makosa ya kigaidi na kufadhiri vitendo vya kigaidi.
#BREAKING: Mahakama imemuachia huru Mbunge Wilfred Lwakatare baada ya DPP kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi yake #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/P37bJg2XwV
— AyoTV (@ayotv_) September 21, 2017
“RPC ni Mtu mdogo siwezi kuzungumza naye, nimempa siku 3” – MUSUKUMA